Faida za kiafya unapokula kwa ‘mfungo’
Written by Black Hot Fire Network on March 21, 2025
KILA mmoja anataka kuimarisha afya ya mwili ili kuwa na afya njema.
Utafiti umeonyesha kuwa moja ya mbinu za kutimiza hilo ni kula kwa saa chache na kisha ‘kufunga’ kwa saa nyingi – kwa Kimombo intermittent fasting.
Mbinu hii ina manufaa sio tu katika kupunguza uzito wa kilo mwilini bali pia hatari ya kupatwa na maradhi yanayotokana na ulaji vyakula duni, kama vile maradhi ya moyo na kisukari.
Hususan kisukari cha aina ya Type 2 diabetes kwa sababu unapofunga kiwango cha sukari kwa damu hupungua na hivyo kupunguza hitaji la mwili kuunda kimeng’enya cha . . .