Firat aweka mastraika benchi Harambee Stars ikisaka ushindi dhidi ya Zimbabwe – Taifa Leo

Written by on September 23, 2024


HARAMBEE Stars ya Kenya imeanza mechi yake ya kwanza ya nyumbani ya kufuzu kushiriki Kombe la Afrika (AFCON) mwaka 2025 dhidi ya Zimbabwe bila mshambulizi katika mechi ya Ijumaa, Septemba 6, 2024.

Kocha Engin Firat aliamua kuanzisha washambulizi Jonah Ayunga (St. Mirren, Scotland), Victor Omune (AFC Leopards), John Avire (Sekka El Hadid, Misri), Benson Omala (Safa, Lebanon) na Alwyn Tera (FC Ararat, Armenia) kitini.

Waliopangwa kufanya majukumu ya kutafuta mabao sasa ni Ronney Otieno Onyango (Gor Mahia) na Eric Johana Omondi (Uta Arad, Romania) kwa sababu mvamizi matata wa Al Duhail, Michael Olunga bado yuko nje akiuguza jeraha.

Kenya iko Kundi J pamoja na Zimbabwe, Namibia na mabingwa mara tano Cameroon.

Timu mbili za kwanza kutoka kundi hili ndizo zitaingia AFCON 2025 nchini Morocco moja kwa moja.

Harambee Stars (wachezaji 11 wa kwanza):

Kipa – Byrne Omondi (Bandari FC);

Mabeki – Joseph Stanley Okumu (nahodha/Reims – Ufaransa), Sylvester Owino Ahono (Gor Mahia), Alphonce Otieno Omija (Gor Mahia), Erick Ouma Otieno (Rakow, Poland);

Viungo – Anthony Akumu Agay (Kheybar, Iran), Austine Odhiambo Otieno (Gor Mahia), Duke Ooga Abuya (Yanga SC, Tanzania), Richard Odada (Dundee United, Scotland), Ronney Otieno Onyango (Gor Mahia), Eric Johana Omondi (Uta Arad, Romania).

Wachezaji wa akiba:

Kipa – Levis Opiyo (AFC Leopards), Patrick Matasi (Kenya Police);

Mabeki – Abud Omar (Kenya Police), Amos Nondi (FC Ararat, Armenia), Sharif Majabe (Bandari FC);

Viungo – Kenneth Muguna (Kenya Police), Chrispine Erambo (Tusker);

Washambulizi – Jonah Ayunga (St. Mirren, Scotland), Victor Omune (AFC Leopards), John Avire (Sekka El Hadid, Misri), Benson Omala (Safa, Lebanon) na Alwyn Tera (FC Ararat, Armenia);

Kocha – Engin Firat (Uturuki)



Source link


Reader's opinions

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *



Current track

Title

Artist