Furaha riboribo Kenya Police wakiandikisha historia na kutwaa KPL – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on June 15, 2025
Fowadi wa Kenya Police David Simiyu akiwania mpira na kipa wa Shabana Maxwel Mulili (kushoto) mnamo Juni 15, 2025 wakati wa mechi za Ligi Kuu (KPL). PICHA|CHRIS OMOLLO
Kenya Police Jumapili waliandikisha historia kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu (KPL) baada ya kuwa ligini kwa misimu minne.
Baada ya kupandishwa KPL mnamo 2021, Kenya Police walishinda ubingwa baada ya kuichapa Shabana 1-0 katika uga wa Kenyatta, mjini Machakos.
Brian Okoth aliwaamsha mashabiki wa Kenya Police baada ya kuruka juu na kufunga mpira wa kichwa mnamo dakika ya 75.
