Hawa ndio walisuka ndoa ya Ruto na Raila – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on September 23, 2024
Rais William Ruto (kulia) na Bw Raila Odinga walipokutana nchini Uganda nyumbani kwa Rais Yoweri Museveni. PICHA | MAKTABA
WANDANI wakuu wa kinara wa upinzani Raila Odinga waliohusika katika makubaliano na Rais William Ruto, walifanya msururu wa mikutano usiku kabla ya rais kutangaza hadharani majina ya mawaziri wateule, Taifa Leo imebaini.
Kakaye mkubwa Odinga, Oburu Oginga, aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju, Kiranja wa Wachache Bungeni Junet Mohamed, Bw Joe Ager na Profesa Adams Oloo walishiriki mazungumzo yaliyoishia katika uteuzi wa viongozi wa ODM . . .