Kahawa inaongezea wazee nguvu – Watafiti – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on September 23, 2024
Kahawa moto kwenye kikombe. PICHA|HISANI
UNYWAJI wa kahawa unasaidia katika kuimarisha misuli ya mwili miongoni mwa wanaume wakongwe, Wanasayansi wamebaini.
Wengi ambao wametinga ukongwe huwa na tatizo la misuli yao kuisha nguvu au kulegea, ugonjwa ambao unafahamika kwa kimombo kama ‘Sarcopenia’.
Ugonjwa huo hulemaza uwezo wa mwanaume kuwajibikia majukumu ya kawaida hata kazi nyumbani baada ya kutinga uzee (wale ambao wana umri wa miaka 60 na zaidi) kwa sababu misuli yao huisha nguvu.
Kati ya mambo ya kawaida ambayo mtu hawezi kufanya akiwa na ugonjwa huo ni kutaabika . . .