Kenya kuandaa fainali, Tz mechi ya ufunguzi, UG wakiangukia ‘makombo’ CHAN – Taifa Leo

Written by on June 19, 2025

Uga wa Kasarani ulipokuwa ukikarabatiwa. PICHA|HISANI

FAINALI ya Kombe la Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya nyumbani maarufuku kama CHAN itasakatwa Kenya.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Jumanne lilitangaza kuwa fainali hiyo sasa itagaragazwa uga wa MISC Kasarani mnamo Agosti 30.

Mechi ya kwanza na sherehe ya ufunguzi wa kipute hicho kinachoonza Agosti 2 hadi Agosti 30 nayo itasakatwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam Tanzania.

Hii ina maana kuwa hata sherehe ya ufunguzi ya CHAN itafanyika kwenye uga wa Benjamin Mkapa, Tanzania.



Current track

Title

Artist