Mihic akiri presha inamlea, Gor ikiendea Mara Sugar KPL leo – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on April 27, 2025
Kocha mpya wa Gor Mahia Sinisa Mihic akiringisha jezi yake mnamo Februari 3, 2025. Picha|Hisani
KOCHA wa Gor Mahia Sinisa Mihic Jumamosi alikiri kuwa presha inaendelea kumlemea katika juhudi za klabu ya kutetea taji lake la Ligi Kuu (KPL).
Mihic, 48 amekiri kuwa wakiendelea kudondosha alama, basi watajipata pabaya na kupoteza taji hilo ambalo Gor imelichukua mara 22.
Mihic atarejea kwenye benchi ya kiufundi ya Gor Jumapili baada ya kukosa sare ya 1-1 dhidi ya Sofapaka na kupigwa 1-0 na limbukeni FC Talanta mnamo Alhamisi uga huo huo . . .