Mtihani mgumu kwa UDA Mlimani
Written by Black Hot Fire Network on June 22, 2025
TANGAZO la mwenyekiti wa Devolution Empowerment Party (DEP) Lenny Kivuti kwamba chama hicho kitaunga mkono chama cha Democratic Party (DP) katika uchaguzi mdogo wa kuwania kiti cha ubunge cha Mbeere Kaskazini limefasiriwa kama pigo juhudi za UDA kutwaa kiti hicho.
Mnamo Mei 11, mwaka huu, katika mojawapo ya ziara zake nyingi katika Kaunti ya Embu, Naibu wa Rais Prof Kithure Kindiki aliapa kuhakikisha kuwa chama hicho tawala kinatwaa kiti hicho.
“Nitapiga kambi katika eneo la Mbeere Kaskazini hadi UDA ishinde. Serikali imerejesha kiti cha uwaziri katika eneo hili. Watu wa Mbeere wanafaa kushukuru kwa kumpigia kura . . .