Mwandamanaji ashtakiwa kuvunja Bunge na kuiba CCTV za Sh2.2 milioni – Taifa Leo

Written by on July 10, 2024

Kevin Mwamiri Mang'are akiwa mahakama ya Milimani Julai 10, 2024 aliposhtakiwa kuvunja jengo la Bunge na kuiba mitambo ya kamera za CCTV za thamani ya Sh2,275,000. Picha|Richard Munguti

MWANDAMANAJI ameshtakiwa kwa kuvunja jengo la Bunge la Kitaifa na kuiba kutoka mle ndani vifaa vya kielektroniki vya thamani ya Sh2.2 milioni.

Kevin Mwamiri Mang’are alishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi wa mahakama ya Milimani Bw Gilbert Shikwe.

Mang’are alikana mashtaka matatu ya kuvunja na kuingia katika jengo la bunge mnamo Aprili, Mei na Juni 2024.Current track

Title

Artist