Nairobi United yalenga fainali ya Mozzart Bet ikivaana na Mara Sugar leo – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on June 14, 2025
Kocha wa Nairobi United Nicholas Muyoti awali akiwa Nairobi City Stars. PICHA|HISANI
Nairobi United itakuwa ikilenga kuandikisha historia kufika fainali ya Kombe la Mozzart Bet itakapovaana na Mara Sugar kwenye mechi ya nusu fainali itakayogaragazwa Jumapili uga wa Dandora, Nairobi.
Timu hiyo ndiyo pekee isiyokuwa ya Ligi Kuu (KPL) ambayo imebakia kwenye kipute hicho ambacho mshindi hufuzu Kombe la Mashirikisho Afrika (Caf) na pia kushinda Sh2 milioni.
Mshindi wa mechi hiyo ya nusu fainali atachuana na Gor Mahia kwenye mchuano wa fainali katika tarehe ambayo itatangazwa baadaye mwezi huu.
