Polisi hawana sababu zozote za kisheria kumpiga mtu – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on June 18, 2025
Polisi akimkimbiza mwandamanaji katika maandamano yaliyopita. Ukatili wa polisi unamulikwa. Picha|Maktaba
UTAKAPOSHIKWA na polisi nchini Kenya kisha uzabwe kofi – na nakuombea lisiwe la kukuua – jua mara moja kwamba maisha yako yamo hatarini.
Kisa na maana? Isipokuwa tu nia ya kujitoa hasira zake mwenyewe, kisheria, ofisa wa polisi nchini Kenya hana sababu yoyote ya kukupiga. Haafikii lengo lolote kwa kutumia nguvu dhidi yako. Pengine nia yake kukuadhibu kinyume cha sheria.
Zamani polisi wetu waliwapiga washukiwa ili kuwalazimisha kukiri makosa, lakini baadaye sheria zetu zilibadilika ikawa kwamba taarifa yoyote unayoandikisha kwa polisi . . .