Ruto si Zakayo, wa Biblia alikuwa msikiza ushauri – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on October 30, 2024
Rais William Ruto. Picha|Maktaba
Rais William Ruto amelinganishwa na Zakayo wa Bibilia Takatifu ambaye alikuwa mtoza ushuru mkuu.
Ruto amehalalisha matumizi ya jina hilo nchini na hata ughaibuni. Katika sherehe za kuadhimisha siku ya wafanyikazi duniani kwa kinywa chake, aliwakumbusha Wakenya kuwa wamuite Zakayo na vinginevyo watatoa ushuru.
Watu wakasema Zakayo ashuke. Inavyoonekana bado hajashuka na hamna dalili ya kufanya hivyo. Ndiyo sababu nasema huyu si Zakayo, kama ni Zakayo basi ana moyo mgumu kupita . . .