Unga wa watoto uliochakatwa wavutia masoko ng’ambo – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on September 23, 2024
Edwin Mairo wakati wa maonyesho ya Sankalp 2024 Jijini Nairobi. PICHA|SAMMY WAWERU
EDWIN Mairo na Everlyne Alpha ni wajasiriamali wenye hadithi ya kuvutia, ambapo safari yao kuzindua kampuni ya kuchakata unga ilianza kwa uchuuzaji.
Wawili hao ndio waasisi wa Gemini Flour Mills, kampuni ya kusindika mseto wa unga iliyoko Changamwe, Kaunti ya Mombasa.
Ilizinduliwa mwaka 2017, Mairo akifichua kwamba walianza kwa kuchuuza unga.
“Tulikuwa tukichuuza unga wa nafaka mbalimbali kwenye mitaa ya mabanda, na hatimaye tukagundua familia nyingi watoto wao wameathirika na kero ya Utapiamlo,” anasema . . .