Wakenya mawindoni ng’ambo kusaka mkwanja marathon mbalimbali – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on April 5, 2025
Isaiah Lasoi aongoza wenzake mbio za 10km wakati wa mashindano ya AK ya Idara ya Magereza mnamo Desemba 2022. Atashiriki Prague Half Marathon wikendi hii. PICHA | CHRIS OMOLLO
LILIAN Kasait na Isaiah Lasoi wanapigiwa upatu kufanya kweli Jumamosi watakapotimka Prague Half Marathon nchini Czech, katika wikendi yenye shughuli kibao za kutafuta donge nono na kuimarisha muda kwenye marathon na nusu-marathon mbalimbali.
Wawili hao wana muda bora kuliko wapinzani wao kwenye mbio hizo za kilomita 21 ambazo zimevutia washiriki 16,000. Lasoi anajivunia kukamilisha umbali huo kwa dakika 58 na sekunde . . .