Wanyonyi avuna Sh12.9 milioni kutoka Grand Slam Track nchini Jamaica – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on April 7, 2025
Bingwa wa Olimpiki mbio za mita 800, Emmanuel Wanyonyi. PICHA|HISANI
BINGWA wa Olimpiki mbio za mita 800, Emmanuel Wanyonyi ameongeza Sh12.9 milioni (Dola za Amerika 100,000) kwenye akaunti yake baada ya kuibuka mshindi wa mbio za 800m/1,500m kwenye mashindano ya Grand Slam Track mjini Kingston, Jamaica yaliyofanyika Aprili 4-6, 2025.
Wanyonyi alimaliza 1,500m katika nafasi ya kwanza na nambari mbili katika 800m.
Katika 1,500m, Wanyonyi alibwaga majina makubwa – bingwa wa Olimpiki Cole Hocker, bingwa wa dunia Josh Kerr na mshindi wa nishani ya . . .