Familia yaomboleza jamaa yao aliyeuawa na ‘teargas’ – Taifa Leo
Written by Black Hot Fire Network on June 27, 2024
Waandamanaji katika barabara za Nairobi. Picha|Billy Ogada
VIJANA walipojitokeza kuandamana dhidi ya Mswada wa Fedha 2024/25 katikati mwa jiji la Mombasa Jumanne, familia ya Emmanuel Giggs Tata, 20, haikuwahi kufikiria angekuwa sehemu ya takwimu za watu waliopoteza maisha yao katika maandamano hayo.
Emmanuel alikuwa na wenzake katikati ya mji wa Mombasa, dakika chache kabla ya polisi kuwafyatulia vitoa machozi ili kutawanya waandamanaji.
Kulingana na Bw Mwasa Nzamba, ambaye ni binamuye marehemu, kifo chake kilitokea muda mchache baada . . .