Sports

Wajir All Stars, Wajir Queens mabingwa wa Safaricom Chapa Dimba Kaskazini Mashariki mwa Kenya NA TOTO AREGE WAJIR All Stars ndio mabingwa wa Safaricom Chapa Dimba Kanda la Kaskazini Mashariki mwa Kenya, baada ya kuinyoa Lyon 04 FC kutoka kaunti ya Garissa 2-0 katika fainali iliyopigwa Jumapili, Februari 25, 2024 katika Chuo Kikuu cha Garissa. […]

Kenya yapoteza mwanariadha mwingine, Charles Kipsang NA LABAAN SHABAAN KENYA imefiwa na mwanariadha mwingine, Charles Kipsang Kipkorir, majuma mawili baada ya kifo cha mshikilizi wa rekodi ya marathon duniani Kelvin Kiptum. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Xinhua, Kipsang alifariki Jumamosi, Februari 24, 2024 nchini Cameroon. Alianguka na kufa muda mfupi baada ya kumaliza […]

Arsenal, Man City katika presha ya kujaza pengo lililofunguliwa na Liverpool LONDON, UINGEREZA MANCHESTER City na Arsenal watakuwa mawindoni kupunguza presha ya kuachwa na Liverpool kwenye Ligi Kuu (EPL) watakapopepetana na Bournemouth na Newcastle leo usiku, mtawalia. Nambari mbili Man-City wana alama 56, nne nyuma ya viongozi Liverpool. Wana mtihani unaokaa rahisi dhidi ya wenyeji […]

Wito kwa serikali, Nike kujenga miundomsingi ya riadha dunia ikimuaga Kiptum NA HASSAN WANZALA VIONGOZI mbalimbali wametoa wito kwa serikali na kampuni za vifaa vya michezo kuwajali wanariadha ili kupiga jeki juhudi zao za kuizolea Kenya sifa na medali katika ulingo wa spoti. Wakiongea Ijumaa wakiwa Chepkorio katika hafla ya ibada kabla ya mazishi ya […]

Arsenal waliolipua Burnley Jumamosi wakosa risasi katika Uefa NA MASHIRIKA PORTO, URENO: KAMBI ya Arsenal imejaa masikitiko baada ya kupigwa bao moja chungu na FC Porto dakika ya mwisho katika mechi ya duru ya kwanza ya raundi ya 16-bora kwenye soka ya Klabu Bingwa Ulaya nchini Ureno, Jumatano. Vijana wa kocha Mikel Arteta walikuwa wameshinda […]

Bondia anayeinukia Lamu afichua ‘bullying’ ilimzindua kujijenga NA KALUME KAZUNGU MARA nyingi mtu hujipata akifanya vyema kwenye mchezo fulani, iwe ni kandanda, raga, netiboli, magongo, voliboli, tenisi, na masumbwi kutokana na mapenzi aliyo nayo kwenye mchezo husika. Wengine hujipata hodari na kutia bidii kwenye nyanja fulani, hasa punde anapogundua kuwa fani hiyo ni talanta yake […]

Kiptum alifariki kutokana na majeraha ya kichwa – Upasuaji NA TITUS OMINDE KWA muda wa saa tano, mwanapatholojia wa serikali Johansen Oduor amekuwa makini akifanya uchunguzi wa kina kwa mwili wa marehemu mshikilizi wa rekodi ya mbio za Marathon Kelvin Kiptum katika hospitali ya Eldoret mnamo Jumatano. Dkt Oduor alithibitisha muda mfupi baadaye kuwa Kiptum […]

Mbappe apuuza Arsenal, Man Utd na Chelsea na kuyoyomea Real Madrid PARIS, UFARANSA SASA ni rasmi mshambuliaji matata Kylian Mbappe ataondoka Paris Saint Germain (PSG) ya Ligue 1 na kujiunga na Real Madrid ya La Liga nchini Uhispania. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 25 tayari ameijulisha PSG kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu huu hapo […]

AFCON2023: Ivory Coast na Nigeria wamwagia wachezaji mamilioni na nyumba za kifahari NA JOHN ASHIHUNDU MARAIS wa nchi za Ivory Coast na Nigeria wametoa pongezi na zawadi nono za mamilioni ya pesa pamoja na nyumba kwa wachezaji waliowezesha timu za nchi hizo kutinga fainali ya Afcon iliyochezwa Februari 11, 2023 ugani Alassane Quattara Stadium. Mbali […]

Chesi: Chipukizi Robert Mcligeyo aingia katika kikosi cha timu ya taifa NA TOTO AREGE MCHEZAJI chipukizi wa mchezo wa chesi Robert Mcligeyo kwa mara ya pili mfululizo, amefanikiwa kuingia kwenye kikosi cha taifa kama mchezaji bora. Uteuzi wa mwisho wa timu ya taifa ulikamilika mwishoni mwa wiki jana, katika KCB Club jijini Nairobi, huku Mcligeyo, mwenye […]


Current track

Title

Artist