Karua apuuza ‘madharau ndogondogo’ ya Kalonzo kusema hatoshi mboga – Taifa Leo

Written by on March 22, 2024

Karua apuuza ‘madharau ndogondogo’ ya Kalonzo kusema hatoshi mboga

NA WANDERI KAMAU

KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua, Ijumaa alipuuzilia mbali kauli ya kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kwamba hatoshi mboga kuuongoza mrengo wa Azimio la Umoja-One Kenya.

Kwenye ujumbe alioandika katika mtandao wa X (zamani ukiitwa Twitter), Bi Karua alisema wapigakura ndio watakaoamua kuhusu kiongozi watakayemchagua uchaguzi utakapofika.

Kauli ya Bi Karua inafuatia taarifa iliyochapishwa na gazeti la Taifa Leo, Ijumaa, ambapo Bw Musyoka alisema kuwa kiongozi huyo hajatimiza vigezo vya kuuongoza mrengo . . .



Current track

Title

Artist