Kipruto azima Kipchoge na kuvunja rekodi mbio za Tokyo Marathon – Taifa Leo

Written by on March 3, 2024

Kipruto azima Kipchoge na kuvunja rekodi mbio za Tokyo Marathon

NA GEOFFREY ANENE

BENSON Kipruto amelambisha sakafu Eliud Kipchoge akitawala mbio za Tokyo Marathon nchini Japan, Jumapili, Machi 3, 2024.

Katika raundi hiyo ya kwanza ya Marathon Kuu Duniani (WMM), bingwa wa Boston Marathon 2021 na Chicago Marathon 2022 Kipruto alikata utepe wa kwanza baada ya kukamilisha umbali huo wa kilomita 42 kwa saa 2:02:16. Muda wake bora katika 42km ulikuwa 2:04:02 kutoka Chicago Marathon 2023 kwa hivyo ameuimarisha kwa dakika moja na sekunde 46.Current track

Title

Artist