Kocha De Boer ashauri Zirkzee apuuze Man United ajiunge na Arsenal – Taifa Leo

Written by on May 24, 2024

Kocha De Boer ashauri Zirkzee apuuze Man United ajiunge na Arsenal

KOCHA wa zamani wa Uholanzi, Frank de Boer ameomba Mholanzi mwenzake Joshua Zirkzee achague Arsenal FC badala ya Manchester United akiamua kuondoka Bologna nchini Italia katika kipindi kirefu cha uhamisho kinachofunguka Juni 14 hadi Septemba 2.

Mshambulizi Zirkzee amechangia pakubwa katika kampeni za Bologna msimu huu, akiisaidia kujikatia tiketi ya kushiriki Klabu Bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia yao.



Current track

Title

Artist