Korti yazima polisi kutumia vitoa machozi na ukatili dhidi ya waandamanaji – Taifa Leo

Written by on June 28, 2024

Lori la polisi linalorushia waandamanaji maji ya kuwasha. Picha|Sila Kiplagat

MAHAKAMA Kuu Ijumaa Juni 28, 2024 ilitoa agizo la kuzuia polisi ya kitaifa kutumia maji ya kuwasha na vitoa machozi dhidi ya waandamanaji wanaodumisha amani.

Maafisa wa polisi waliamriwa kusimamisha matumizi ya risasi, risasi za mpira, silaha butu na hatua nyingine kali dhidi ya waandamanaji.

Mahakama Kuu pia iliagiza maafisa wa usalama wanaosimamia waandamanaji kuacha kutumia nguvu za kikatili au aina yoyote ya ghasia au  mauaji yoyote kinyume cha sheria.

Vile vile, Mahakama Kuu iliamuru polisi kusitisha kukamata . . .



Current track

Title

Artist