Mnatoza ushuru na hamlipi madaktari, Kalonzo aishangaa serikali – Taifa Leo

Written by on March 22, 2024

Mnatoza ushuru na hamlipi madaktari, Kalonzo aishangaa serikali

NA WYCLIFFE NYABERI

KIONGOZI wa Wiper Kalonzo Musyoka ameitaka serikali ya Kenya Kwanza kuwalipa madaktari ili wasitishe mgomo wao.

Bw Musyoka alishangaa utawala wa sasa unatoza ushuru mwingi hivyo hakuna kisingizio kwamba hakuna rasilimali za kutosha.

Alisema hayo Alhamisi akiwa katika mji wa Nyamira

Alidai Rais William Ruto ni kama analemewa na majukumu yake.

“Madaktari wanagoma takribani wiki mbili sasa. Wamelemeza huduma za afya. Wamesimama kidete na wanafunzi wa udaktari ambao wamemaliza masomo yao lakini hawajaajiriwa kazi . . .



Current track

Title

Artist