Umuhimu wa watoto wadogo kupata usingizi wa kutosha – Taifa Leo

Written by on April 6, 2024

Umuhimu wa watoto wadogo kupata usingizi wa kutosha

NA MWANDISHI WETU

WAKATI pacha wake James Mwema (aliomba jina libadilishwe) walikuwa wanazaliwa, ilikuwa siku njema maishani mwake.

Hata hivyo, walipofikisha umri wa miezi mitatu na nusu, pacha hao hawakuwa wanalala ipasavyo mchana na hata usiku.

“Walikuwa wanalala tu kwa dakika thelathini na iwapo mmoja wao angeamka na aanze kulia, mwenzake angefuata. Usiku vilevile, walikuwa wakiamka angalau mara kumi au kumi na mbili,” anakumbuka.



Current track

Title

Artist